Shirika la bidhaa za kudhibiti wadudu aak-GROW limewahakikishia Wakenya kwamba bidhaa zote za dawa za kuua wadudu katika soko la humu nchinii ni salama na zinadhibitiwa kikamilifu. Mkurugenzi Mtendaji Joel Mutai anabaini kuwa kila bidhaa iliyoidhinishwa hupitia miaka mingi ya utafiti wa kisayansi, majaribio makali, na uchunguzi huru wa udhibiti na Bodi ya Bidhaa za Kudhibiti Wadudu. Anaongeza kuwa marufuku ya baadhi ya dawa za kuua wadudu barani Ulaya hayatumiki kiotomatiki nchini, kwani PCPB hutathmini kwa uhuru usalama, ufanisi, na athari za mazingira na afya za kila bidhaa kabla ya kuidhinishwa au kupigwa marufuku.
JOEL MUTAI - TECHNICAL