Chama cha ODM kinatarajiwa kuanza ziara ya siku tatu katika Kaunti ya Turkana leo, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kumuenzi kiongozi wa chama hicho, marehemu Raila Odinga. Ziara hiyo itahusisha mikutano na wananchi mashinani pamoja na mikutano ya hadhara huko Kataboi, Lodwar, Lokichogio, Kakuma na Kalokol. Shughuli hizo zitahitimishwa Jumapili kwa ibada kanisani na mkutano wa hadhara huko Kalokol.
VOX POP – TURKANA