Madereva jijini Nairobi wanapaswa kujiandaa kwa kufungwa kwa barabara kuanzia usiku wa manane wikendi hii, huku jiji likijitayarisha kwa mbio za 'Standard Chartered Nairobi Marathon' za mwaka 2026 zitakazofanyika Jumapili. Kamanda wa Trafiki wa Kaunti ya Nairobi, Joseph Chirchir, anasema maafisa wa polisi na wasimamizi wa trafiki watatumwa ili kudhibiti mtiririko wa magari na kuhakikisha usalama wa wakimbiaji. Takriban washiriki 30,000, wakiwemo wanariadha 1,000 kutoka mataifa ya nje, wanatarajiwa kushiriki.
JOSEPH CHIRCHIR – CLOSURE