Rais William Ruto ameanzisha upya mashambulizi yake dhidi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtuhumu kwa kusaliti makubaliano yao ya kisiasa. Akizungumza katika Kaunti ya Uasin Gishu, Ruto aliregelea tena mzozo wake na Uhuru, akidai rais huyo wa zamani alikuwa ameahidi kuunga mkono azma yake ya urais baada ya kutumikia mihula miwili. Ruto alimshutumu Uhuru kwa kumtelekeza alipotafuta urais mwaka wa 2022, akisema rais mstaafu badala yake aliwasihi Wakenya wasimchague.

WILLIAM RUTO - BURE