Mama Ida Odinga ataongoza sherehe ya kimataifa ya kuwasha mishumaa katika Kang'o Ka Jaramogi kesho kuadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga. Kamati ya uongozi ya ukumbusho, inayoongozwa na Adams Oloo, ilisema tukio hilo litaanza saa kumi na mbili jioni, likiwakutanisha Wakenya na wafuasi wa Raila duniani kote. Kamati hiyo iliwasihi Wakenya na marafiki wa kiongozi huyo marehemu kuwasha mishumaa popote walipo, ikiwa ni pamoja na nyumba, makanisa, misikiti na mikusanyiko ya kijamii, kwa heshima ya urithi wake.
IDA ODINGA - FLAME