Gavana wa Homa Bay, Gladys Wanga, amesisitiza tena umoja wa chama cha ODM, akisema kuwa chama hicho bado kina nguvu licha ya madai ya kudhoofika kufuatia kufariki kwa kiongozi wake wa zamani, Raila Odinga. Akizungumza huko Teso Kusini, Kaunti ya Busia, Wanga aliwahimiza wakaazi kuendelea kuenzi mchango na urithi wa Raila kwa kukiunga mkono chama hicho, huku akionyesha imani kuwa ODM itahifadhi viti vyote vya kaunti ya Busia. Pia, alitetea ushirikiano wa chama hicho na serikali ya Rais Ruto.
GLADYS WANGA – ODM