Mtu mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya ukuta kuporomoka katika eneo la ujenzi huko Athi River Kusini, Kaunti ya Machakos. Marehemu, Mbata Mutinda mwenye umri wa miaka 34 alifariki alipowasili katika Hospitali ya Shalom, ambapo wenzake waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu na hali zao ni thabiti. Polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa ukuta huo.