Watu walio karibu na uongozi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) wanajadili pendekezo la kuongezwa kwa muda, idadi ya timu katika Ligi Kuu ya Kenya hadi kufikia 19 kwa msimu wa 2026/27. Iwapo pendekezo hilo litakubaliwa, hakutakuwa na mechi za mchujo (playoff), na timu zote mbili, Kariobangi Sharks na Mombasa United, zitashiriki ligi hiyo kuu kwa msimu husika. Ligi hiyo itarejea katika muundo wake wa kawaida wa timu 18 kuanzia msimu wa 2027/28. Hatua hii inafuatia mvutano wa kisheria ambapo timu ya Sharks, ambayo ilishushwa daraja, inasisitiza kuwa inastahili kucheza mechi ya mchujo dhidi ya Mombasa United ili kuamua ni ipi itakayobaki katika ligi kuu.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Garissa, Mandera na Moyale.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.