Mbunge wa Belgut, Nelson Koech, ameihimiza serikali kuchukua hatua madhubuti dhidi ya waandaaji na wahusika wa ghasia katika mikutano ya kisiasa. Akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen, Koech alisema ghasia za kisiasa zinaweza kudhibitiwa kwa kuwawajibisha wanasiasa wanaopanga au kufadhili vitendo hivyo. Alipendekeza kuwazuia wanasiasa watakaopatikana na hatia kugombea nyadhifa za kuchaguliwa, ikiwa ni hatua ya kuzuia ghasia wakati wa kampeni za kisiasa.
NELSON KOECH – HOLD