Seneta wa Kisii, Richard Onyonka, amepinga madai ya Rais William Ruto kwamba upinzani hauna ajenda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza katika mahojiano ya televisheni ya asubuhi, Onyonka alisema upinzani unatekeleza wajibu wake wa kikatiba kwa kuchunguza miradi ya serikali na kuhoji gharama zake. Alisisitiza kuwa upinzani una mpango mbadala kwa ajili ya nchi, huku akiongeza kuwa serikali ina uwezo wa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa vile inasimamia rasilimali za nchi, tofauti na upinzani.
RICHARD ONYONKA –CRITICIZE