Rais William Ruto ametetea mfumo uliopendekezwa na serikali wa kufadhili elimu ya juu kupitia mikopo pekee, akisema utazingatia zaidi uwezo wa kitaaluma wa wanafunzi badala ya hali ya kifedha ya wazazi wao. Akizungumza wakati wa kukabidhi Barua ya Ruhusa ya Muda kwa Chuo Kikuu cha Kamagambo, Ruto alisema mfumo huo umebuniwa ili kufanya ufadhili wa elimu ya juu uwe wa haki zaidi na endelevu kwa muda mrefu.