Muungano wa Wananchi kuhusu Mageuzi ya Uchaguzi, ulioitishwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi na Mbunge Caroli Omondi, unatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari jijini Nairobi asubuhi ya leo. Muungano huo utafanya mkutano huo habari katika hoteli moja jijini Nairobi, huku majadiliano yakitarajiwa kuzingatia mageuzi ya uchaguzi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao.