Tume ya NCIC inasema itatoa maelekezo wiki ijayo baada ya kuwaita viongozi kadhaa kwa madai ya matamshi ya chuki. Makamu mwenyekiti wa tume hiyo Irene Tulel anasema miongoni mwa walioitwa ni Gavana wa Busia Paul Otuoma, Mbunge wa Kitutu Masaba Clive Gisairo na Mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma. Tume hiyo inasema inabaki macho, haina upendeleo na imara katika kutekeleza mamlaka yake, ikiongeza kuwa njia mwafaka ya kusonga mbele itawasilishwa baada ya majadiliano.

IRENE TULEL - SUMMONS