Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wakuu wa Shule za Upili nchini Willie Kuria amepinga madai kwamba serikali imetoa kikamilifu fedha za shule za upili kwa muhula wa sasa. Kuria alisema shule zimepokea Sh14,000 kwa kila mwanafunzi dhidi ya Sh22,000 zinazotarajiwa kila mwaka. Aliitaka Wizara ya Elimu kutoa fedha hizo zilizobaki haraka ili kusaidia shughuli za shule na kuzuia usumbufu wa masomo.

WILLIE KURIA - CAPITATION