Tume ya EACC imewahimiza raia kushiriki kikamilifu katika kulinda rasilimali za umma kwa kuripoti madai ya ufisadi. Wakizungumza huko Nakuru wakati wa kongamano la ushiriki wa umma kuhusu bajeti ya fedha ya 2026/27, wakaazi waliibua wasiwasi na kupendekeza hatua za kukabiliana na ufisadi na mwenendo usio wa kimaadili katika serikali ya kitaifa na za kaunti. Maafisa wa EACC walisisitiza kwamba ushirikiano wa umma ni muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora.
KIPSANG’ SAMBAI - BITE