Malkia Strikers wataendelea na ulinzi wao wa taji dhidi ya Algeria katika robo fainali ya Mashindano ya Voliboli ya Wanawake ya Mataifa ya Afrika ya mwaka 2026 katika uwanja wa ndani wa Kasarani usiku wa leo. Wenyeji Kenya ambao wanafukuzia taji lao la 11 la bara watawategemea mashabiki wao wa nyumbani kutwaa taji hilo. Mechi hiyo itaanza saa moja usiku na itatanguliwa na Cameroon dhidi ya Uganda, Rwanda dhidi ya Ghana na derby ya Afrika Kaskazini kati ya Misri na Tunisia. Nahodha Meldina Sande na Mariana Sokoiyo wamewasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono.
MELDINA SOKOIYO - MALKIA
Nahodha wa zamani wa Cameroon Zambo Anguissa ametangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa. Katika taarifa yake, kwenye mitandao yake ya kijamii, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 alisema kuvaa jezi ya Indomitable Lions ilikuwa ndoto ya utotoni na anaondoka uwanjani kwa fahari. Anguisa ambaye alikosa AFCON ya mwaka huu kutokana na jeraha alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda taji la AFCON la 2017 na pia kumaliza wa tatu mwaka wa 2021 huko Yaunde. Alicheza mechi 66 kwa Cameroon na kufunga mabao matano.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.