Barcelona waliregea tena katika nafasi ya juu kwenye jedwali la La liga kwa ushindi wa 5-2 dhidi ya Rayo Vallocano katika Nou Camp jana usiku. Lamin Yamal na Rafinha walifunga mabao mawili kila mmoja huku Florian Lejuene akijifunga, na Sergio Camello akifunga mabao mawili ya faraja kwa Vallocano. Barca ambao wanatetea taji lao waliwatoa wapinzani wao Real Madrid kutoka kileleni wakiwa na pointi tisa sawa na Madrid lakini wakiwa na tofauti ya mabao. Mechi nyingine ya siku ya tatu ilishuhudia Osasuna ikiishinda Getafe 1-0.
Manchester City wamekubali mkataba wenye thamani ya hadi pauni milioni 65 kumsajili Iliman Ndiaye kutoka Everton. Makubaliano ya winga huyo wa Senegal yana thamani ya pauni milioni 65. Tottenham walikubali masharti na Everton Ijumaa usiku kwa Ndiaye, wakati ilionekana kana kwamba Richarlison angehamia huko kwingine. Hata hivyo, Richarlison alishindwa kukubaliana masharti binafsi na klabu yake ya zamani ya Everton. Wakati huo huo, City wameanzisha mazungumzo na Chelsea katika azma yao ya kumsajili kiungo Enzo Fernandez.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.