Wakenya wenye vitambulisho ambavyo havijachukuliwa wanahimizwa kuvichukua huku mbio za kisiasa za mwaka 2027 zikianza. Mtaalamu wa utawala Javas Bigambo anasema kitambulisho ni muhimu si tu kwa kupata huduma bali pia kwa usajili wa wapiga kura na ushiriki katika uchaguzi. Bigambo anasema maafisa wa utawala wa serikali wanapaswa kuimarisha uhamasishaji wa umma na kuwafikia waombaji kupitia machifu na manaibu wao ili kuhakikisha vitambulisho vinachukuliwa kabla ya uchaguzi wa 2027.
JAVAS BIGAMBO - IDS