Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa na Real Madrid, Karim Benzema, ameondoka katika klabu ya Saudi Pro League ya Al Hilal baada ya miezi sita tu. Klabu hiyo yenye makao yake makuu Riyadh ilitangaza kwamba mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, ambao ulikuwa umesalia na mwaka mmoja, ulisitishwa kwa makubaliano ya pande zote mbili. Hii inakuja siku moja baada ya Al Hilal kukamilisha usajili wa pauni milioni 51 wa mshambuliaji wa Uingereza Ollie Watkins kutoka Aston Villa. Mshindi huyo wa Ballon d'Or wa 2022 na mshindi mara tano wa Ligi ya Mabingwa akiwa na Real Madrid alijiunga na Al Hilal mwezi Februari akitokea kwa timu nyingine ya Saudi Arabia, Al Ittihad.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Mombasa, Kilifi na Malindi.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.