Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Mawasiliano, imetoa wito wa kupanuliwa na kubadilishwa kwa vituo vya kidijitali kote nchini ili kuunda fursa za ajira na ujasiriamali kwa vijana. Wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya kidijitali katika maeneo bunge ya Kilifi na Likoni, mwenyekiti wa kamati hiyo John Kiarie alisema vituo hivyo vinapaswa kutoa ujuzi wa kidijitali unaoweza kuuzwa, upatikanaji wa kazi mtandaoni na majukwaa kwa vijana kuendeleza biashara.

JOHN KIARIE - HUBS