Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi amemkosoa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa madai ya kushindwa kuhakikisha maendeleo ya kitaifa yanawiana wakati wa uongozi wake. Akizungumza na wakaazi wa Malava, Kaunti ya Kakamega, Wandayi alisema Magharibi mwa Kenya imefaidika pakubwa na miradi ya maendeleo tangu Rais William Ruto aingie madarakani mwaka wa 2022, huku akimtuhumu Uhuru kwa kupuuza baadhi ya maeneo wakati wa uongozi wake.
OPIYO WANDAYI - MAENDELEO