Nahodha wa Harambee Stars, Michael Olunga, alitoka benchi na kuifungia Al Arabi dhidi ya klabu yake ya zamani, Al Duhail, huku timu hizo mbili zikitoka sare ya 1-1. Hili lilikuwa bao la kwanza la Olunga katika miezi sita baada ya kupata jeraha la paja lililohitaji upasuaji mwezi Aprili. Olunga amekuwa nje ya kikosi cha kocha mkuu wa Stars, Benni Mc Carthy, na anatarajiwa kurejea, kwa ajili ya mechi muhimu za kufuzu kwa AFCON 2027 dhidi ya Eritrea, Guinea na Afrika Kusini katika kundi D.


Mabingwa wa zamani Misri walijihakikishia nafasi katika michuano ya voliboli ya wanawake ya Afrika kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi jana katika uwanja wa ndani wa Kasarani. Wamisri waliwazidi nguvu Warundi kwa seti 25-7, 25-13 na 25-5, na kujikatia tikiti ya kupambana Tunisia katika robo fainali baada ya wapinzani hao wa Afrika Kaskazini kuishinda Mali 3-0. Wakati huo huo, Rwanda iliishinda Burkina Fasso 3-0 na itapambana na Ghana ambayo iliishinda Zambia 3-1. Wenyeji Malkia Strikers wataendelea na utetezi wao wa ubingwa dhidi ya Algeria kesho baada ya kuifunga Nigeria 3-0, huku Cameroon ikipambana na Uganda.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.