Wafanyakazi wa UHC huenda wakakosa mishahara mwezi Septemba isipokua fedha zilizotengwa kama ruzuku ya masharti zihamishiwe kwa Wizara ya Afya. Waziri wa Afya Aden Duale anasema Wizara hiyo kwa sasa haina fedha za kuwalipa wafanyakazi kwa mwezi Septemba. Anasema mishahara ya Julai na Agosti tayari imelipwa, lakini wizara itahitaji ruzuku ya masharti ili kukidhi mishahara ya Septemba.


ADEN DUALE – SALARIES