Asilimia tisini ya Wakenya wanajua kuhusu shinikizo la damu, huku asilimia 78 wakielewa Kielelezo cha Uzito wa Mwili (BMI) na asilimia 63 wakijua kolesteroli, Utafiti mpya uliofanywa na Doctors for healthy living umebaini. Hata hivyo, utafiti wa watu wazima 1,100 wa mijini na pembezoni mwa miji unaonyesha kwamba licha ya ufahamu mkubwa wa viashiria muhimu vya afya, ni Wakenya wachache wanaovifuatilia mara kwa mara. Matokeo hayo yanaonyesha mapengo katika huduma ya afya ya kinga na tabia ya kutafuta afya.
ROBERT MATHENGE –PRESSURE