Washukiwa wawili wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho kufuatia kukamatwa kwao na timu ya mashirika mbalimbali katika eneo la South B jijini Nairobi. Maafisa kutoka NACADA na Huduma ya Kitaifa ya Polisi walivamia maduka kwenye barabara ya Plains view huko Starehe na kupata mikanda na vifuko vya dawa za kulevya zinazoshukiwa, karatasi za Rizla na mizani ya kidijitali. Vielelezo vyote vilihifadhiwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga huku uchunguzi ukiendelea.
LEACKEY ILLA - ARREST