Kenya Police Bullets ilifuzu kwa fainali za Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF 2026 baada ya kuilaza Yei Joint ya Sudan Kusini 5-0 katika nusu fainali jijini Kigali, Rwanda, jana. Martha Amunyolete alifunga mabao mawili kwa upande wa Police, kabla ya Tereza Engesha, Lorna Nyarinda na Rebecca Okwaro kuongeza moja kila mmoja. Police Bullets sasa itakutana na Kawempe Muslim Ladies katika fainali ya Jumatatu baada ya mabingwa hao wa Uganda kuishinda CBE FC ya Ethiopia 3-0 katika nusu fainali nyingine. Mshindi wa fainali za kesho atafuzu kwa ligi ya mabingwa ya Wanawake ya CAF.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.