Mtaalamu wa utawala Javas Bigambo anasema vitambulisho 173,811 ambavyo havijachukuliwa vinaweza kuwa na athari kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi cha Kenya cha mwaka 2027. Anasema wale wasio na vitambulisho hawawezi kujiandikisha kama wapiga kura, na kuwanyima fursa ya kushiriki katika kuchagua viongozi. Bigambo anasema ingawa raia lazima wachukue vitambulisho vyao, wasimamizi wa serikali wanapaswa pia kuboresha uhamasishaji na juhudi za ufuatiliaji.
JAVAS BIGAMBO - ELECTIONS