FKF imetangaza kwamba Ligi Kuu ya Kenya itaanza kesho, baada ya mahakama ya Muranga kutoa ruhusa Ijumaa. Wageni 3K FC watakabiliana na Mara Sugar katika uwanja wa Embu kabla ya Mathare United kuwakaribisha APS Bomet katika uwanja wa Police sacco. Mabingwa Gor Mahia wataanza utetezi wao wa taji dhidi ya Muranga Seals katika uwanja wa Nyayo Jumanne, huku Migori Youth wakipambana na Police FC katika uwanja wa Awendo huku Ulinzi Stars wakiwakaribisha Tusker katika uwanja wa Ulinzi. Jumatano Nairobi United watawakaribisha KCB, huku Posta Rangers wakipambana na Shabana nayo AFC Leopards wakikaribisha Bandari katika uwanja wa Nyayo.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.