Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot ameitetea IEBC dhidi ya mashambulizi ya kisiasa yanayoendelea. Akizungumza huko Saboti, Kaunti ya Trans Nzoia, Cheruiyot alisisitiza kwamba taasisi huru na zinazoaminika zinasalia kuwa msingi wa mchakato wowote wa uchaguzi wa amani, uwazi na wa kidemokrasia wa kweli nchini, akihimiza upinzani kuipa muda wa kutosha tume ya uchaguzi kutekeleza mamlaka yake ya kikatiba.
AARON CHERUIYOT – IEBC