Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ameahidi kuchukua hatua kali za kisheria kufuatia kufukuzwa kwa wakaazi kutoka Kijiji cha Jipe/Mwakoshemi katika Kaunti ya Taita Taveta. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kisiasa katika kaunti hiyo, Kalonzo alilaani vikali kuhamishwa kwa watu na kuwahakikishia wakaazi kwamba timu yake ya kisheria itapigania kupata haki na kulinda umiliki wao halali wa ardhi.

KALONZO MUSYOKA – LEGAL