Malkia Strikers watakabiliana na Nigeria saa moja usiku katika raundi ya 16 ya michuano ya voliboli ya Afrika inayoendelea katika uwanja wa ndani wa Kasarani. Mabingwa hao watetezi wako kileleni mwa kundi A kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Mali baada ya ushindi mwingine wa 3-0 dhidi ya Zambia katika mechi yao ya ufunguzi Jumanne. Wakati huo huo, Uganda itakabiliana na DR Congo saa saba mchana kabla ya Algeria kucheza na Senegal saa kumi jioni. 




Jua linashuhudiwa Nakuru, Nyahururu na Nyeri.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.