Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatoa wito wa usaidizi mkubwa wa kimataifa ili kudhibiti mkurupuko wa Ebola, akionya kwamba jamii zilizoathiriwa hazipokei msaada wa kutosha. Guterres anasema shughuli muhimu za kukabiliana na janga hilo zinaweza kukosa fedha wakati zinavyohitaji kupanuka. Anaomba dola bilioni moja zilizobaki zinazohitajika kufadhili kikamilifu mpango wa kukabiliana na janga hilo la kibinadamu, akihimiza jamii ya kimataifa kuchukua hatua kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
ANTONIO GUTERRES – EBOLA