Mahakama Kuu huko Murang’a kesho itaamua ombi la FKF linalotaka kuondoa amri zilizosimamisha kuanza kwa ligi wikendi hii. FKF, kupitia timu yake ya kisheria, iliitaka mahakama kuruhusu ligi kuanza Jumamosi, ikisema kwamba kucheleweshwa kwingine zaidi kutakuwa na athari kubwa kwa maandalizi ya vilabu kwa msimu mpya. Kesi hiyo iliwasilishwa na Evans Nduta, ambaye anapinga ombi hilo, na uhalali wa Sheria za FKF za 2025 zilizotumika kwa msimu wa 2025/26.

Malkia Strikers wataendelea na ulinzi wao wa taji dhidi ya Mali katika kundi A, huku Mashindano ya Voliboli ya Wanawake ya Afrika yakiingia siku ya pili katika uwanja wa ndani wa Kasarani jioni ya leo. Wenyeji walikuwa na siku ya mapumziko jana, baada ya kuishinda Zambia 3-0 Jumanne. Ushindi wa Malkia utawashuhudia wakinyakua nafasi ya robo fainali, wanapokaribia taji lao la 11 na tiketi ya michezo ya Olimpiki ya Los Angeles ya mwkaa 2028. Mzuiaji wa kati Marian Sokoiyo ana uhakika wa ushindi.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Kajiado na Narok.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.