Mamlaka ya ubora wa bidhaa nchini KEBS imetoa wito kwa mataifa ya Afrika kuainisha kanuni za biashara ili kuongeza biashara ya ndani ya Afrika, ambayo kwa sasa ni asilimia 17 pekee. Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa Shirika la Viwango la Afrika huko Mombasa, Mkurugenzi Mkuu wa KEBS Esther Ngari alibaini kuwa mifumo ya udhibiti iliyogawanyika inaendelea kuzuia biashara ya mpakani. Ngari alisema kwamba viwango vya kitaifa vinavyokinzana husababisha mvutano usio wa lazima, na hivyo kukatisha tamaa usafirishaji huru wa bidhaa kote barani.


ESTHER NGARI - STANDARDISATION