Chama cha Soka cha Ireland kimeondoa uungwaji mkono wake kwa rais wa Fifa, Infantino. Chama hicho kinasema ni wakati wa mabadiliko na hawatampigia kura Infantino kuchaguliwa tena mwaka ujao. Infantino amekuwa akichunguzwa zaidi tangu jaribio lake la kutaka kuuza asilimia 21 ya hisa katika shughuli za kibiashara za Fifa kwa kampuni binafsi, kukataliwa. Mipango hiyo ilifutwa baada ya ukosoaji mkubwa, huku Uefa ikitishia kususia mashindano yote ya Fifa. Chama cha Soka cha Uingereza, Wales, Scotland na Serbia pia zimeondoa uungwaji mkono wao.

 

Stan Wawrinka anasema ushindi wake wa US Open utakuwa mojawapo ya nyakati bora zaidi maishani mwake baada ya kukosa wildcard ya kushirikihuko New York. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 atastaafu mwishoni mwa mwaka huu na alipewa kadi ya wildcard katika Australian Open na Wimbledon, huku akifikia droo kuu ya French Open katika nafasi. Alifika raundi ya tatu huko Melbourne na kupoteza mechi mbili za raundi ya kwanza huko Paris na Wimbledon mtawalia.



Jua linashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.