Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa miguu ya wanaume walio chini ya umri wa miaka 23, imepangwa dhidi ya Tanzania katika raundi ya ufunguzi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya umri wa miaka 23 mwaka wa 2026. Emerging Stars, itapambana na majirani zao Tanzania katika raundi ya kwanza jijini Nairobi tarehe 28 mwezi ujao kabla ya kusafiri hadi Dar es Salaam kwa raundi ya marudiano tarehe 6 Oktoba. Mshindi wa jumla atakabiliana na Ivory Coast katika raundi ya pili ya kufuzu, huku Tunisia au mshindi kati ya Benin na Gabon, wakisubiri raundi ya mwisho.
Malkia Strikers walifungua utetezi wao wa taji la Mashindano ya Voliboli ya Afrika kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Zambia katika uwanja wa ndani wa Kasarani jana usiku. Mabingwa hao mara 10 wa Afrika wakiongozwa na nahodha Maldina Sande waliwashinda Waafrika Kusini kwa seti 25-14, 25-9, na 25-11. Katika Kundi B, Uganda iliishinda Senegal 3-0 huku mabingwa wa zamani Misri wakiwashinda Burkina Faso 3-0, na Cameroon ikapata ushindi kama huo wa 3-0 dhidi ya Ghana, DRC, Congo iliishinda Burundi 3-0 huku Tunisia ikitoka nyuma na kuishinda Nigeria 3-1.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisii, Kitale na Kericho.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.