Hazina ya Hustler imetoa zaidi ya Sh bilioni 90 huku Wakenya zaidi ya milioni 27 wakipata mikopo kutoka kwa hazina hiyo. Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya anasema angalau watu milioni mbili hukopa kutoka kwa mfuko huo kila siku. Ili kuwezesha kila Mkenya kupata nafasi ya kutafuta mikopo ya kifedha, serikali ilibadilisha sera kutoka kuwaweka walio na deni kwenye blacklist hadi kurekebisha kustahili kwao kwa mikopo.
WYCLIFFE OPARANYA – OPARANYA