Rais William Ruto ameagiza kwamba zaidi ya Watoa Huduma za Afya za Jamii  elfu 107 wajumuishwe katika mpango wa Mamlaka ya Afya ya Jamii ifikapo Jumatatu, huku mpango wao wa marupurupu ukipitiwa upya ifikapo Disemba. Akiwahutubia katika Mkutano wa Afya katika ukumbi wa KICC, Ruto alisema watapokea ujumbe mfupi kutoka kwa wizara ya afya ukithibitisha mpito wao. Zaidi ya hayo, Rais aliagiza kwamba mpango wa SHIF pia uwahudumie wanafamilia wa walengwa.

WILLIAM RUTO - SAJILIWA