Kenya itahitaji dawa zote zinazoingia nchini ziwe na kitambulisho cha kipekee cha kimataifa kuanzia Januari 1, mwaka ujao, chini ya agizo la serikali linalolenga kuimarisha ufuatiliaji na uthibitishaji. Dkt. Joyce Wamicwe, Kiongozi wa Kiufundi wa Afya ya Kidijitali na Taarifa katika taasisi ya Afya ya Kidijitali, alisema shirika hilo linashirikiana na Bodi ya Famasia ili kuhakikisha dawa zinazoagizwa kutoka nje zinatambuliwa na kufuatiliwa kwa njia ya kipekee katika mnyororo mzima wa usambazaji. Alizungumza wakati wa Mkutano wa Afya wa Kenya jijini Nairobi.

JOYCE WAMICWE - IDENTIFY