Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula anasema Bunge litaendelea kuunga mkono mageuzi ya afya ya serikali kupitia sheria, ugawaji wa rasilimali na usimamizi. Akizungumza katika Mkutano wa Afya wa Kenya, Wetang'ula aliangazia sheria nne za afya zilizotungwa mwaka wa 2023, ikiwa ni pamoja na Sheria za SHA na Afya ya Kidijitali. Anasema zaidi ya Wakenya milioni 30 sasa wamesajiliwa chini ya mfumo mpya wa bima ya afya, ikilinganishwa na takriban milioni nane chini ya NHIF.

MOSES WETANGULA - REFORMS