Droo ya mashindano ya 36 ya Driftwood 7s ilifanyika jana, huku mkondo wa nne wa Msururu wa kitaifa ya raga wa Sportpesa ukielekea Mombasa wikendi ijayo. Viongozi wa mashindano KCB ambao wametoka kushinda Kabereri sevens wataanza utetezi wao wa taji dhidi ya Blak Blad, Kisumu RFC na timu ya Emerging 7s ya Uganda katika Kundi B. Kenya Harlequin, Kabras RFC, Nondescripts na wenyeji Mombasa wanakamilisha Kundi A, huku Menengai Oilers, Daystar Falcons, Mwamba na Chuo Kikuu cha Masinde Muliro wakikamilisha Kundi D.
Toleo la 23 la Shirikisho la Michezo ya Shule za Upili za Afrika Mashariki jana lilipigwa jeki na ksh milioni 11.6 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki. Mashindano hayo, yanayoendelea sasa Morogoro, Tanzania, yamevutia timu 413 na washiriki 5,548 kutoka kote Afrika Mashariki wakishindana katika taaluma 51 za michezo. Meneja wa Nchi wa benki hiyo Tanzania, Stephen Wambura ambaye aliongoza uzinduzi huo anasema mashindano hayo ni jukwaa zuri kwa programu za maendeleo endelevu za benki hiyo.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.