Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo amelaani ongezeko la matumizi ya vurugu katika siasa, ikiwa ni pamoja na kuajiri wahuni na madai ya matumizi mabaya ya polisi kuvuruga mikutano ya hadhara. Akizungumza jijini Nairobi, aliwasihi wanasiasa, hasa wale walio katika serikali mpana, kutafuta uungwaji mkono wa wapiga kura kupitia sera na ushawishi badala ya vitisho, vurugu, au mashambulizi dhidi ya wapinzani na wafuasi wao.

MILLIE ODHIAMBO - WIN