Takwimu za ajira zinaonyesha kuwa Kenya iliunda takriban ajira milioni 3.27 kati ya mwaka 2022 na 2025, huku nyingi zikiundwa katika sekta isiyo rasmi. Kulingana na takwimu za shirika la takwimu nchini, nchi hii iliunda ajira 816,600 mwaka wa 2022, 848,000 mwaka wa 2023, 782,000 mwaka wa 2024 na 822,100 mwaka wa 2025. Kati ya jumla hii, takriban ajira milioni 2.84, au asilimia 87, ziliundwa katika sekta isiyo rasmi, huku takriban ajira 420,000 zikiwa za kisasa au rasmi.