Viongozi wa kisiasa na kidini katika Kaunti ya Murang'a wameitaka serikali kuanzisha hazina maalum kwa ajili ya wanaume, wakisema kwamba wameachwa nyuma katika programu za uwezeshaji ambazo kwa kiasi kikubwa zimewalenga wanawake na vijana. Viongozi hao wakiongozwa na Profesa Peter Kagwanja wanasema hazina hiyo itasaidia kushughulikia changamoto za kiuchumi zinazowakabili wanaume wengi na kurejesha nafasi yao katika jamii.
PETER KAGWANJA – MEN