Kiungo wa kati wa Uganda Allan Okello amekamilisha uhamisho wake kwenda AS FAR Rabat ya Morocco kwa ada ya uhamisho ya dola milioni 1.2. Uhamisho huo unawakilisha faida kubwa kwa mabingwa wa Tanzania, ambao walimsajili Okello kutoka Vipers kwa dola 300,000 miezi minane iliyopita. Okelo ambaye alifunga mabao 14 kwa Yanga, alicheza mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo katika Community Shield, katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao Simba wiki iliyopita. Yanga imemrudisha Stéphane Aziz Ki kujaza pengo lililoachwa na Okelo.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.