Seneta wa Kiambu Karungo Thang'wa amelaani shambulio la wikendi iliyopita dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua huko Nakuru, akitaka uvumilivu wa kisiasa kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao. Thang'wa amemsihi Naibu Kiongozi wa Chama cha Jubilee Fred Matiang'i kumdhibiti Mbunge wa Nakuru Town West Samuel Arama, ambaye amehusishwa na machafuko hayo. Arama amekana kuhusika kokote katika tukio hilo. Thang'wa anasema tofauti za kisiasa hazipaswi kuruhusiwa kusababisha vurugu.
KARUNGO THANG’WA – ATTACK