Waziri wa Fedha John Mbadi amepuuza madai kwamba ruwaza ya 2060 ni mradi binafsi wa Rais William Ruto, akisema mpango huo wa maendeleo wa muda mrefu utaundwa kupitia ushiriki wa umma. Mbadi alisema mazungumzo ya kitaifa yatawapa Wakenya, viongozi wa upinzani na wadau wengine fursa ya kuchangia mawazo kuhusu vipaumbele vya kiuchumi na maendeleo ya nchi, akisisitiza kwamba ruwaza hiyo haitashinikizwa na rais.

JOHN MBADI - INFORM