Wapelelezi huko Masinga, Kaunti ya Machakos, wameanzisha uchunguzi baada ya mabaki ya binadamu yanayoaminika kuwa ya mwanamke kupatikana kwenye kisima katika kijiji cha Mukengesya. Mabaki hayo yaligunduliwa Jumatatu wakati mfanyakazi wa shamba alipofungua kisima na kugundua harufu mbaya. Alipoingia ndani, aliona gunia moja kubwa na magunia matatu madogo yakielea ndani ya maji. Polisi walitembelea eneo la tukio ambapo walisema kisima hicho kilikuwa kimefungwa kwa kifuniko cha chuma, ingawa kufuli ilipatikana ikiwa imevunjwa.