Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku ameitwa na NCIC kwa madai ya matamshi ya uchochezi. Gavana huyo anatarajiwa kufika mbele ya tume hiyo tarehe 17 mwezi huu. Kesi ya Ole Lenku inatokana na matamshi aliyotoa alipokuwa akihutubia wakazi wa Ewuaso Oonkidongi katika eneo bunge la Kajiado Magharibi. Kulingana na NCIC, gavana huyo aliwataka Wamaasai kuongoza katika uwakilishi wa kisiasa huko Kajiado na Narok, huku akipinga juhudi za vyama vya siasa za kuteua wagombea kutoka jamii zingine kwa nafasi katika kaunti hizo mbili.