Mpenzi anayedaiwa kuwa wa Gianni Infantino alipewa malipo ya kuondoka kazi kutokana na uhusiano huo, na Uefa, alipokuwa katibu mkuu wake, kulingana na uchunguzi wa Daily Telegraph. Msemaji wa rais huyo wa sasa wa Fifa aliripotiwa kuliambia gazeti hilo Infantino "anakanusha vikali madai haya yasiyo ya kweli". Uefa, ambayo Infantino alikuwa katibu mkuu wake kuanzia 2009 hadi 2016, ilitoa taarifa ikithibitisha "malipo ya kuondoka yalifanywa kwa mtu husika". Madai hayo yanakuja huku Infantino akipigania mustakabali wake kama rais wa Fifa kufuatia mipango yake ya kuuza hisa katika Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi ambayo haikufanikiwa.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Kakamega na Eldoret.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.